Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. PHILIP MPANGO ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika kuipatia Tanzania mkopo nafuu kwa ajili ya kujenga barabara ya njia NNE kuanzia MOROGORO hadi DODOMA ili kuboresha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo.
Dkt. MPANGO ametoa ombi hilo Jijini DODOMA alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo anayewakilisha nchi nane za ukanda wa Afrika Mashariki AMOS CHEPTOO