Tanzania kuingiza dawa za kutibu corona kutoka Madagascar

0
734

Serikali ya Tanzania ina mpango wa kutuma ndege nchini Madagascar kwa ajili ya kubeba dawa za kutibu ugonjwa wa corona.

Rais John Magufuli amesema tayari serikali ya Madagascar imeiandikia barua serikali ya Tanzania kuhusu  dawa hiyo, hivyo serikali imeona ni vema ikaileta nchini kwa ajili ya kuwasaidia watanzania.

Amesisitiza kuwa serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha watanzania wote wanaougua corona wanapata msaada stahiki kulingana na uwezo wa serikali.

Rais Magufuli ameyasema hayo wilayani Chato mkoani Geita wakati wa hafla ya kumuapisha Dkt Mwigulu Nchemba kuwa waziri wa Katiba na Sheria kuchukua nafasi ya Balozi Augustine Mahiga ambaye amefariki dunia.