Serikali ina mpango wa kuzalisha mbegu za mazao mbalimbali, ambazo zitauzwa kwa wakulima kwa bei nafuu
Mpango huo wa Serikali umetangazwa mkoani Tabora na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, wakati wa mkutano wa hadhara ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akiwahutubia wakazi wa mkoa huo.
Amesema hivi karibuni wakulima nchini wataanza kununua mbegu zitakazozalishwa hapa nchini badala kuagiza kutoka nje, na kwamba serikali imetenga
shilingi bilioni 80 kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu hizo.
Katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini waziri Bashe amesema, Serikali imetenga tani elfu 65 za mbegu za alizeti zitakazogawiwa kwa wakulima ili walime kwa wingi zao hizo na hivyo kusaidia kupatikana kwa mafuta ya kutosha.