Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Mazrui wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Geneva Balozi Hoyce Temu walipotembelea katika Ofisi za Uwakilishi wa Tanzania nchini Uswisi.
Mawaziri hao wapo Geneva kuhudhuria Mkutano wa 75 wa Afya Duniani unaendelea nchini Uswisi.
Ujumbe wa Tanzania unahudhuria mkutano huo na mikutano ya pembezoni inayohusiana na masuala ya Afya.