Tamko la vyama 9 vya upinzani kuhusu uchaguzi mkuu 2020

0
427

Vyama gisa vya upinzank vimetoa tamko la kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 28, 2020 na mgombea wa CCM, Dkt. John Magufuli kuibuka mshindi baada ya kupata 84.4% ya kura zote.

Katika tamko lao, vyama hivyo vimempongeza mgombea huyo kwa kushinda na kusema kwamba mambo aliyoyafanya ndani ya miaka mitano iliyopita yamechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wake.

Vyama hivyo pia vimeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuratibu uchaguzi huo uliohusisha vyama 15.