TAMISEMI yaomba Trilioni 9 mwaka 2023/2024

0
133

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 yenye jumla ya shilingi Trilioni 9.1 kwa ajili ya ofisi hiyo.

Kati ya fedha hizo shilingi Trilioni 5.7 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumuisha mishahara na shilingi Trilioni 1.06 kwa ajili ya matumizi mengine.

Shilingi Trilioni 3.5 zimeombwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo shilingi Trilioni 2.4 ni fedha za ndani na shilingi Trilioni 1.12 ni fedha za nje.