Tamisemi : Dugange hajajiuzulu

0
139

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema kuwa,
Naibu Waziri (TAMISEMI)
anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange ambaye pia ni
Mbunge wa jimbo la Wang’ingombe mkoani Njombe hajajiuzulu nafasi hiyo.

TAMISEMI imetoa taarifa hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema kuwa Dkt. Dugange amejiuzulu wadhifa wake ili kupisha uchunguzi.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imesisitiza kuwa taarifa hiyo ni uzushi na ipuuzwe, kwani Dkt. Dugange bado ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI na
kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma kufuatia ajali ya gari aliyoipata Aprili 26, 2023.