Katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani katibu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mtaa(TALGWU) Mkoa wa Songwe Emanuel Alfonce ameiomba serikali kuwafikiria wafanyakazi katika ongezeko la mishahara
Aidha Alfonce ameongeza kuwa chama cha wafanyakazi kipo tayari kupinga rushwa makazini zinazokuwa sababu ya kurudisha nyuma jitihada za wafanyakazi kuwahudumia wananchi
Katika hatua nyingine Alfonce pia amesema chama hicho kipo tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha zoezi zima la sensa ya watu na makazi linafanikiwa.