TAKUKURU yafikisha saba mahakamani

0
560

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU mkoa wa Manyara imewafikisha mahakamani watumishi saba wa mkoa huo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara, Isdori Kyando amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya upendeleo wa zabuni ya ujenzi wa Rest House ya mkoa huo na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya shilingi.

Watumishi saba akiwemo aliyekuwa meneja wa Wakala wa Majengo Nchini – TBA mkoa wa Manyara wamefikishwa katika Mahakama ya mkoa wa Manyara wakituhumiwa kugawa Zabuni ya ujenzi wa Rest House ya Mkoa kwa upendeleo kwa Kampuni ya Wulkan Engineering Limited hali iliyoisababishia hasara serikali.