Rais John Magufuli ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa Nchini (TAKUKURU) kufanya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, watu wote walioshiriki kuhujumu miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri 82 nchini.
Rais Magufuli pia amekabidhi taarifa ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, ili akaichambue na kuchukua hatua kwa kila aliyehusika katika kukwamisha miradi hiyo.
Akihutubia katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa huko mkoani Lindi, Rais Magufuli amesema kuwa hakuna mtu atakayebainika kukwamisha miradi hiyo na kuachwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Rais Magufuli ameagiza kupatiwa taarifa ya uchunguzi wa TAKUKURU, ili aweze kufanya maamuzi kwa Viongozi ambao watabainika kukwamisha miradi iliyotiliwa shaka na Mwenge wa Uhuru mwak
