Tahadhari ya kimbunga Jobo yaendelea kutolewa

0
137

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini  (TMA)  imeendelea kutoa tahadhari kwa Wakazi wa maneno ya mwambao wa bahari ya Hindi,  kutokana na kuwepo kwa tishio la kimbunga Jobo.

TMA imewakumbusha Wakazi hao kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo ikiwemo ile inayowataka kutokaa chini ya majengo marefu na miti mirefu ili kuepuka madhara endapo kimbunga hicho kitapiga kwenye  maeneo hayo ya mwambao wa bahari ya Hindi.

Kimbunga Jobo kilichoripotiwa tarehe 20  mwezi huu , kwa siku ya leo kimeonesha mwelekeo wa kuelekea kisiwa cha Mafia mkoani Pwani.