Tabora watakiwa kuchangamkia fursa za uchumi

0
372

Wananchi wa mkoa wa Tabora wametakiwa kuchangamkia fursa za uchumi zinazopatikana mkoani humo.

Wito huo umetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wazawa kupata fursa za kufanya biashara pamoja na ajira.

Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amesema mkoa wa Tabora una mazingira mazuri kwa ajili ya kilimo na kwamba serikali imeweka mkazo kwenye sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji kwa kuwa wananchi wengi wamejiajiri kwenye sekta hizo.

Pia amewahimiza Watanzania kutunza chakula kilichopo kutokana na uhaba wa mvua mwaka huu na kuwataka kulima mazao yanayostahimili mvua kidogo..

Rais Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara yake ya siku tattu mkoani Tabora ambapo amezindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.