Taasisi za Kidini Kanda ya Ziwa kuhakikiwa

0
180

Taasisi za Kidini na Jumuiya za Kijamii zilizopo Kanda ya Ziwa zitaanza kuhakikiwa kuanzia Oktoba Saba hadi 18 mwaka huu.

Uhakiki huo ambao unafanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni wa awamu ya Nne na unaihusisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Geita na Kagera.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeeleza kuwa, uhakiki huo utafanyika katika Ofisi zilizoandaliwa, ambazo zipo kwenye jengo la Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.