Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Kapteni Mstaafu George Mkuchika, amezipongeza taasisi za dini nchini kwa kujitoa kushiriki katika kutoa huduma za kijamii kwa watanzania.
Kapteni Mstaafu Mkuchika ametoa pongezi hizo katika kilele cha Jubilee ya miaka 75 ya Shirika la Masista wa chama cha Mariam Mtakatifu CMM wa Kanisa la Angalikana Tanzania Dayosisi ya Masasi.