Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye amesema kuwa lengo lake kuu la kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni kukipa nguvu chama hicho kwa kuwa na Viongozi bora na sio bora Viongozi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Sumaye amesema kuwa, kuna haja ya kuwa na Demokrasia ya kweli katika vyama vya Siasa nchini hasa katika namna ya kuwapata Viongozi.
Akizungumzia uchaguzi wa Viongozi wa chama hicho kwa Kanda, Sumaye amesema kuwa kwa maoni yake Kamati Kuu ya chama hicho haikufuata Demokrasia ya kweli hasa katika nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho ngazi ya Taifa.
Aidha Sumaye amesema kuwa, safari yake ya kugombea nafasi hiyo ameisitisha na kuuomba Uongozi wa juu wa CHADEMA kuondoa makundi ndani ya chama chama hicho.