Spika Ndugai asifu kuongezeka kwa mapato ya Madini

0
193

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema tokea kuingia Kwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli Tanzania imeanza kunufaika na Sekta ya Madini.

Spika Ndugai ameyasema hayo Leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya ufungaji wa Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ambapo amewataka wadau kushirikiana na Serikali kuhakikisha wadau, Serikali pamoja ma watanzania Kwa ujumla wananufaika na rasilimali hiyo ya madini ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu na kueleza kuwa atasimamia Bunge tukufu ili kuhakikisha linaweka Sera na kanuni nzuri za madini.