Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), -Hosea Kashimba amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma na kukutana na Spika wa Bunge Job Ndugai.
Wakati wa mazungumzo yao, Spika Ndugai ameeleza kuridhishwa na mwanzo mzuri wa utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo wa PSSSF.
