Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema
Bunge lina mipaka katika kujadili suala la uwekezaji wa bandari na liliishamaliza mjadala huo, hivyo wanachotakiwa kufanya hivi sasa Wabunge ni kuendelea kuwasikiliza Wananchi.
Dkt. Tulia ameweka wazi kuwa Bunge linawakilisha Wananchi na kuishauri Serikali, hivyo kama litaletewa mkataba wa bandari kwa utaratibu mwingine wa kibunge itakuwa ruksa kwa Wabunge kuchangia.
“Waheshimiwa Wabunge tulienda majimboni tumewasikia Wananchi, lakini pia tumewasikia wale wasio wa majimbo yetu wakiendelea kutoa maoni ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Uwekezaji bandari sisi kama Wabunge ni kazi yetu kuendelea kuwasikiliza Wananchi na kuisimamia Serikali.” amesema Dkt. Tulia
Spika Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Agosti 29,2023 mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.