Siri ya Mwalimu Nyerere kusoma vitabu zaidi ya 8000

0
201

“Elimu ni silaha yenye nguvu zaidi unayoweza kutumia kuubadilisha ulimwengu.”

Ni maneno aliyowahi kuyasema mpigania uhuru na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini mwenye asili ya Afrika Hayatii Mzee Nelson Mandela.

Maneno yanayofanana na hayo yamewahi kusemwa na Mwanzilishi wa Taifa la Marekani, Benjamin Franklin na yake ni ‘uwekezaji katika maarifa hulipa riba bora’.

Kauli zote hizo zinajidhihirisha katika makazi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyopo Butiama mkoani Mara ambapo kuna chumba chenye mkusanyiko wa vitabu zaidi ya elfu nane ambavyo Mwalimu licha ya majukumu yake mengi alitumia vema muda wake wa mapumziko kujionngeza maarifa kwa kuvisoma.

Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Madaraka Nyerere amesema, tabia hiyo ya kujisomea vitabu ilimfanya baba yake aonekane ni mtu mwenye akili nyingi na aliyejua kutetea hoja zake.

Ameongeza kuwa kusoma sana vitabu pia kulimsaidia Mwalimu Nyerere kujua mambo mengi yaliyofanywa na wengine hasa Viongozi na au kufahamu namna ora ya kujenga hoja pale anapotakiwa kusimamia hoja zake.

Madaraka anasema Mwalimu Nyerere alisoma kila kitabu alichopewa kama zawadi na vingine vingi, ambavyo kwa sasa vimehifadhiwa katika maktaba hiyo iiliyopo Butiama.

“Alikuwa akipewa zawadi za vitabu mbalimbali naye alikuwa akisoma vitabu vyote vikiwa na mada tofauti tofauti kama vile siasa, kilimo, dini, afya, teknolojia, sayansi na mada zingine nyingi ambazio zilimfanya kujua mambo mengi zaidi na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo kulingana na mada anazosoma kwenye vitabu hivyo.” ameongeza Madaraka Nyerere

Aprili 13 mwaka inatimia miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa Aprili 13 mwaka 1922, ikiwa na maana kiwa angekiwa hai kiongo’i huyo angekuwa na umrii wa miaka 100 kwa maana nyingine umri wa karne moja.