“Ambacho watu hawafahamu, huu mradi wa bomba la mafuta ni wa muda mrefu kidogo. Nilibahatika kufanya kazi kwenye ofisi ya sheria mwaka 2013 ambapo tulishauri Total mwaka huo kuhusu sheria zote za Tanzania ambapo kama bomba lingepita Tanzania.
Wakati huo ushauri huo ulitoka upande wa Kenya nao walipewa maelekezo hayohayo kungalia sheria zimekaaje na Tanzania tulipewa maelekezo hayo kusema sheria zetu zimekaaje.
Ilikuwa ni jambo zuri sana na elimu tosha sababu kwa sisi wanasheria vijana kidogo tukagundua hii sio mara ya kwanza Tanzania inajenga bomba
Bomba la kwanza ni bomba la TAZAMA limejengwa mwaka 1968 kutoka Tanzania kwenda Zambia, bomba lipo hatujawahi sikia madhara yoyote ya kimazingira. Bomba la pili limejengwa na TPDC kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam, la gesi asilia na wote sidhani kama tumewahi kusikia athari zozote kuhusu miradi hiyo”
Amesema Kamanga Kapinga
Mwanasheria anayefuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa Mradi