Simanzi mwili wa Balozi Kijazi ukiwasili Korogwe

0
186

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi umewasili nyumbani kwao Korogwe, Tanga baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2021.

Vilio na majonzi vimetawala miongoni mwa waombolezaji walio pokea mwili wa Balozi Kijazi baada ya kuwasili wilayani humo.

Marehemu Balozi Kijazi anatarajiwa kuzikwa Jumamosi mchana wilayani humo.