Silaha haramu kuteketezwa kesho

0
74

Jeshi la Polisi nchini, kesho litateketeza silaha haramu zilizosalimishwa kwa hiari katika kampeni maalum iliyofanyika nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu hadi Oktoba 31 mwaka huu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime amesema silaha hizo zitateketezwa katika viwanja vya shabaha vya Jeshi Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kunduchi, Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini.