Leo ni Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ambapo watu wengi duniani huiadhimisha siku hiyo kwa kupeana zawadi mbalimbali kama kadi na maua zenye ishara ya upendo.
Siku hiyo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Februari 14 na inaelezwa kuwa chimbuko lake ni Mtakatifu Valentine aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki wa miaka ya 496 baada ya Kristo.