Siku ya Sayari Dunia iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1970, wakati Seneta wa Marekani kutoka Wisconsin alipoitisha maandamano ya kitaifa ili kuongeza ufahamu kuhusu masuala ya mazingira.
Sayari Dunia inaelezwa kuwa ni mahali pa kipekee na pa kushangaza, hivyo unahitajika ushirikiano wa viumbe wote wanaoishi katika sayari hiyo ili kuitunza.
Hiyo ndio sababu Aprili 22 ya kila mwaka zaidi ya watu bilioni moja duniani husherehekea siku ya Sayari Dunia (Earth Day) ili kuilinda sayari dhidi ya mambo kama vile uchafuzi wa mazingira na ukataji miti hivyo na kufanya shughuli kama vile kuzoa taka na kupanda miti lengo likiwa ni kuifanya sayari dunia iendelee kuwa mahali penye furaha na afya kwa kuishi.
Wanasayansi wa Mazingira wanasema unaweza kusherehekea Siku ya Sayari Dunia na kuilinda Sayari hiyo kwa wakati mmoja.