Siku ya Redio Duniani

0
282

Leo ni Siku Redio Duniani, siku ambayo ilianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusherehekea matangazo ya redio na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa miongoni mwa watangazaji wa redio.

Siku ya Redio Duniani ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 2013 kufuatia azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mwaka 2012.