Siku nne za Rais Samia mkoani Mara zatoa matumaini mapya

0
165

Rais Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya siku nne mkoani Mara, pamoja na mambo mengine Rais Samia Suluhu Hassan amezindua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Mbali na kuzindua miradi, Rais Samia pia alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Mara na kufahamu changamoto zilizopo mkoani humo, hali iliyopelekea kukunjua makucha kwa viongozi wa mkoa.

Miongoni mwa eneo alilosisitiza kufanyiwa kazi kwa weledi ni pamoja na wakaguzi wa ndani mkoani humo, kufanya kazi yao ipasavyo kwa kukagua mapema matumizi ya fedha za miradi ya maendeelo ili kuweza kubaini mapungufu mapema katika miradi hiyo kabla haijafikia hatua mbaya.

Agizo hilo amelitoa baada ya kukerwa na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo, ambao unatokana na ubinafsi, mivutano pamoja na kutokuwa na kauli moja kwa baadhi ya Viongozi ndani ya Halmashauri hiyo.

Kuhusu Miradi ya Maji Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi kulinda miradi hiyo kutokana na gharama kubwa za uendeshaji, huku akiwataka Maafisa wa Maji kutowabambikia bili Wananchi.