Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema mkoa wa Tanga umepokea kwa simanzi kubwa sana kifo cha Balozi John Kijazi, kwani amekuwa na mchango katika maendeleo ya mkoa huo.
Aidha, ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumsindikiza kiongozi huyo katika safari yake ya milele.
Balozi Kijazi amefariki Dunia Februari 17, mwaka huu katika hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.