Serikali imetangaza kuwa, kuanzia mwaka huu wa 2019, Sherehe za Uhuru ambazo zimekua zikifanyika Disemba Tisa kila mwaka, zitakuwa zikifanyika Kikanda.
Akihutubia Baraza la Maulid Kitaifa katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa kwa kuanzia Sherehe hizo kwa mwaka huu zitafanyika katika Kanda ya Ziwa na zitafanyika kwenye mkoa wa Mwanza.