Shekhe Alhad: Viongozi wa serikali wanategemea maombi yetu

0
104

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema, ni wajibu wa viongozi wa dini kuwaombea viongozi wakuu wa serikali ili waweze kutimiza majukumu yao kwa weledi.

Ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa kongamano la viongozi wa dini kuhusu sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu

Shekhe Alhad amesemea ushirikiano wa viongozi wa dini katika kuhamasisha sensa ya watu na makazi ni jambo zuri, ambalo litalisaidia Taifa katika kupanga mipango ya maendeleo.

Amewataka waumini wa dini zote nchimi kupuuza wanaobeza juhudi za Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano, na kutaka dini isiwe kigezo cha kugawa umoja na wao.

Shekhe huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ameongeza kuwa lengo la viongozi wa dini kuungana na kushikiana ni kuhakikisha amani inadumishwa nchini na kuhakikksha hakuna vitendo vya uvunjifu wa amani.