Sheikh Alhadi Salum: Tuheshimiane katika tofauti za dini zetu

0
254

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amesema ni vyema kila mtu amfahamu mwenzake katika imani yake ili kutunza amani ya nchi.

Akizungumza katika kongamano la amani la viongozi wa dini jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo amesema, “tunapaswa kuheshimiana katika tofauti zetu za dini ili amani iliyojengwa katika taifa iendelee kudumu wakati wote.”

Tunapozungumzia amani ni jambo kubwa hivyo wagombea wanapaswa kumcha na kumuogopa Mungu ili isije ikafikia viongozi hao wakafanya damu za Watanzania kuwa zulia jekundu la kuwapeleka ikulu.

Pia amewahasa wapiga kura kutumia haki yao ya msingi kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi watakaopewa na Mwenyezi Mungu. Ameihimiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jeshi la Polisi limehimizwa kuhakikisha amani inatawala wakati wote na baada ya uchaguzi.