Shamrashamra za Pasaka hazijakatazwa

0
196

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi halijakataza sherehe za pasaka kama ambavyo alinukuliwa katika taarifa aliyotoa jana.

Masime amesema ujumbe ulivyopokelewa sivyo ulivyomaanishwa bali polisi wanapinga vitendo vya uhalifu kwa siku hiyo.

“Ibada za sherehe za Pasaka kwenye makanisa, sherehe za kifamilia, hitma, familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, sheria , kanuni na taratibu za nchi,” ameeleza Msemaji wa Polisi.

Maadhimisho ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka duniani kwa mwaka huu wa 2021 yanafanyika Jumapili hii, Machi 04.