Shaka: Uchumi wa nchi umefunguka

0
135

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka amesema, mfumo shirikishi kwa wafanyabiashara umesaidia kufungua uchumi ambapo kwa sasa mzunguko wa fedha kwa wafanyabiashara upo vizuri.
 
 
Shaka ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo mkoani Dar es Salaam, ambapo maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanaendelea.
 
 Amesema Chama Cha Mapinduzi kimepokea maoni kutoka kwa wananchi mbalimbali hasa wafanyabiashara, wakieleza kuwa kwa sasa wanaona wepesi wa kufanya biashara zao  kwani mzunguko wa fedha umerejea.
 
 
Shaka ameeleza kuridhishwa na maandalizi ya maonesho ya Sabasaba kwa mwaka huu na kuongeza kuwa maonesho ya mwaka huu  yamegusa mahitaji ya wananchi kwa kuwa washiriki wengi wamebuni utaratibu mpya katika utoaji huduma katika viwanja hivyo vya Sabasaba.