Shaka ato siku 7 kwa viongozi wa soko la Feri

0
95

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ametoa Siku Saba kwa Viongozi wa Soko la Samaki Feri pamoja na Wafanyabiashara katika eneo hilo kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kuangalia namna ya Kutatua Changamoto ambazo zipo kwenye Soko hilo la Samaki.

Shaka ametoa kauli hiyo leo Mei 25, 2022 wakati wa ziara yake katika Soko hilo la Samaki Feri.

Akizungumza na Wafanyabishara wa Soko hilo la Samaki Shaka amewataka kuishi kwa kwa kuzingatia maono, Dira pamoja na uwajibikiaji ambao umekuwa ukisisitizwa na Serikali.

“Nataka niwaambie ndugu zangu, nimetoa Siku Saba ili mkae chini na mmalize changamoto zenu, kisha mtakayo kubaliana Myafikishe Serikalini na Kwenye Ngazi za Chama cha Mapinduzi CCM” amesisitiza Shaka.

Kwa Upande wake mkuu wa Wilaya ya Ilala Ludigija Ng’wilabuzu amemueleza Katibu huyo wa NEC, Itikadi na Uenezi namna ambavyo Serikali imekuwa ikisogeza huduma za Kijamii kwa Wananchi ikiwemo Upatikanaji wa Maji Safi na Salama, huduma za Afya pamoja Uboreshaji wa Sekta ya Elimu.

“Pamoja na hayo Serikali imekuwa ikitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, imekuwa na mpango mzuri kwa ajili ya Wafanyabiashara ndogo ndogo kwa kuwawezesha kupata Fedha zinazotokana na Mikopo inayotolewa kupitia halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam” amesema Ludigija.