Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi kupuuza taarifa kuwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi AgostI mwaka huu kuna kipengele kinachohusu dini.
Amesema jambo hilo halipo na halijawahi kuwepo katika Sensa zote za Watu na Makazi ambazo zimewahi kufanyika nchini.
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa upande wa Zanzibar, ambapo yeye alikuwa ni mgeni rasmi.
Amesema kipengele kipya kilichoongezwa katika Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka huu ni anuani za Makazi na kuwataka Watanzania wote kutoa ushirikiano ili kufanikisha jambo hilo.
Kauli mbiu ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ni kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, jitokeze kuhesabiwa.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.
