Serikali yazizika rasmi paspoti za zamani

0
433

Kuanzia leo Februari Mosi raia yeyote wa Tanzania mwenye paspoti ya zamani (MRP) hatoruhusiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kwa kutumia paspoti hiyo kutokana na serikali kusitisha matumizi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Uhamiaji mtu yeyote anayetaka kwenda nje ya nchi atalazimika kuwa na paspoti mpya ya kielektroniki ndipo aweze kuendelea na safari yake.

Hata hivyo, kwa raia wa Tanzania waliopo nje ya nchi watakaokuwa wanarejea nyumbani kuanzia leo kwa kutumia paspoti za zamani wataruhusiwa kuingia nchini, lakini hawataweza kuzitumia tena kutoka nje ya nchi.

Aidha, zoezi za ubadilishaji na utoaji wa paspoti za kielektroniki linaendelea katika ofisi za uhamiaji zilizopo katika mikoa ya Tanzania, ofisi za uhamiaji Kurasini, Afisi Kuu Zanzibar, na ofisi zote za balozi za Tanzania nje ya nchi.