Serikali yazindua mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya Dawa

0
362

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine 6 za utafi na utoaji mafunzo ya Afya nchini, imezindua mfumo wa udhibiti wa Dawa na tafiti zake.

Mfumo huo ni sehemu ya mradi wa miaka miwili wa ufuatiliaji wa matumizi ya Dawa na tafiti za dawa za binadamu, unaohusisha pia taasisi za utafiti wa Dawa kutoka visiwani Zanzibar.

Akizindua mradi huo Mganga Mkuu wa serikali Dkt. Abel Makubi, amesema serikali inaunga mkono utekelezaji wake na kwamba, utasaidia kuongeza udhibiti wa matumizi ya dawa na tafiti zake.

Akizungumzia Mradi huo utakahusisha pia taaisi za utafiti wa magonjwa ya binadamu na vyuo vinavyotoa elimu ya Afya, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo, amesema mpango huo utawezesha ufuatiliaji wa matumizi ya Dawa kwa wagonjwa hapa nchini.

Taasisi na vyuo vinavyohusika na utekelezaji wa Mradi huo ni pamoja na Chuo Kikuu Kishiriki cha afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili ,(MUHAS) , Chuo Kikuu cha Afya cha Kilimanjaro (KCMC), Taasisi ya utafiti ya Magonjwa ya Binadamu ya Zanzibar (ZARI), Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ya (NIMRI), Mamlaka ya udhibiti wa Dawa Zanzibar, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) na Taasisi ya Utafiti ya nchini Scotland(STP).