Serikali yawaonya watumishi kutovujisha siri/taarifa

0
327

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt  Philip Mpango amelitaka baraza la wafanyakazi wizara hiyo  kufanyakazi kwa kufuata misingi yao na hatasita kumchukulia hatua mtumishi atakayebainika kukiuka misingi na kutoa siri na taarifa nyeti za serikali.

 Dkt. Mpango ameyabainisha hayo jijini Dodoma  wakati alipokuwa akifungua   mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo na kuongeza kuwa mtumishi yeyote atakayekiuka taratibu na miongozo hatavumilika.

“Natanguliza onyo kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kukiuka taratibu, miongozo na miiko ya kazi yake ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango utajutia ukaidi wake.”

Aidha, amewataka wafanyakazi hao kuwa wana majukumu makubwa katika mstakabali wa Taifa hasa wakati huu wa kutekeleza bajeti ya serikali katika majukumu yake.

“Hii ina maana tunaowajibu wa kuongeza tija na ufanisi katika kutekeleza  majukumu yetu na naamini kuwa mtatumia mkutano huu kutathimini utendaji kazi,” amesema.

Pia ametaka viongozi hao kuwa na utaratibu wa kuwasikiliza watumishi ili kupunguza au kuondoa malalamiko  na manung’uniko ya wafanyakazi pindi wanapokuwa kazini ili wafanye kazi kwa utulivu kufikia malengo.

“Lazima tutambue  na kukubali kuwa ufanisi sehemu ya kazi hutegemea uhusiano uliopo baini ya viongozi na wafanyakazi, hivyo basi nawaasa viongozi wenzangu tufanye kila tuwezalo kujenga uhusiano mzuri.”