Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewaagiza wamiliki wa shule zote nchini kutodai ada ya kipindi ambacho wanafunzi hawakuhudhuria masomo kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali kuzuia wanafunzi kwenda shule ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
Waziri Ndalichako amelazimika kutoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya baadhi wa wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule mbalimbali ya kudaiwa ada pindi wanafunzi watakaporejea shuleni.
Aidha Waziri Ndalichako ameziagiza shule zote nchini kufuata maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na wataalamu wa afya ya namna ya kujikinga na virusi vya corona.