Serikali yatoa kongole kwa vituo vya redio

0
305

Katika kuadhimisha Siku ya Redio Duniani hii leo, Serikali imewapongeza wadau wa redio nchini kwa kuendelea kutumia chombo hicho kuwajulisha Watanzania matukio mbalimbali yanayotokea nchini na duniani.

Katika taarifa yake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa, serikali itaendelea kuenzi mchango na kazi nzuri inayofanywa na vituo vya redio nchini.

Aidha, ameongeza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uanzishwaji wa redio nyingi zaidi.

Hadi Februari 12 mwaka huu, jumla ya redio 204 zilikuwa zimesajiliwa ambapo 21 kati ya hizo ni za mtandaoni.