Serikali yataka kufanyika tathmini kwenye maeneo ya migodi

0
563

Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan amesisitiza suala la kufanya tathmini katika maeneo yote ya migodi na kwa wachimbaji wadogo ili kubaini kiwango cha uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jijini Dodoma alipokutana na viongozi pamoja na watumishi waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Amesema tathmini hiyo itaisaidia serikali na taasisi mbalimbali kuchukua hatua sahihi katika kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na watumishi waandamizi wa Ofisi yake pamoja na wale wa NEMC kwa lengo la kujadili hali ya utunzaji wa mazingira hapa nchini.