Serikali yasisitiza Ebola haijaingia nchini

0
243

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa, hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitika kuugua Ebola hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa, taarifa zinazoenezwa kuwa Tanzania kuna ugonjwa huo si za kweli.

Amesema kuwa, wagonjwa walioelezwa awali kuwa wana dalili za Ebola, wamefanyiwa vipimo vyote na kubainika kuwa hawakua na ugonjwa huo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka Watanzania wote kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa ugonjwa huo haujaingia nchini.

Amesisitiza kuwa, serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.