Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, – Job Ndugai ameishauri Serikali kuweka viwango vinavyofanana vya malipo ya posho kwa Watendaji wa Vijiji, Vitongoji, Halmashauri za wilaya na Manispaa ili kuondoa malalamiko yanayotokana na kutofautiana kwa viwango hivyo.
Spika Ndugai ametoa ushauri huo Bungeni jijini Dodoma, wakati akiweka msisitizo kwenye swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Lindi Mjini Hassan Suleiman Kaunje ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itaanza kuwalipa posho Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
https://www.youtube.com/watch?v=iCwcnM8jKN0&feature=youtu.be
Baada ya maswali kadhaa ya nyongeza pamoja na majibu kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara, Spika Ndugai akaitaka Serikali kutaja viwango vinavyofanana vya malipo kwa Watendaji hao badala ya kuwa na viwango tofauti.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri Waitara amesema kuwa, kwa sasa malipo kwa ajili ya Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji, Mitaa,
Vitongoji na Miji yanategemea makusanyo ya Halmashauri husika.