Serikali yasema hakutakua na mgao wa umeme

0
202

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewahakikishia Watanzania kuwa hadi sasa mabwawa ya kuzalisha umeme ya Mtera na Kidatu yana maji ya kutosha, hivyo hakutakuwa na mgao wa umeme.

Dkt Kalemani ameeleza hayo baada ya kukagua bwawa la kuzalisha umeme la Mtera ambalo kwa sasa limejaa maji, na serikali kuamua kuyafungulia kabla hayajaleta madhara.

Amewataka Wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni karibu na mto Ruaha Mkuu na Kilombero yalikofunguliwa maji kuondoka katika maeneo hayo, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Akitoa maelezo ya kina cha maji cha bwawa la Mtera, Meneja wa Kituo hicho Mhandisi Mathew Mwagomba amesema kuwa, machi Ishirini mwaka huu kina cha maji kilikua kimefikia mita za ujazo 698.74, kiasi ambacho ni kikubwa.

Bwawa la kufua umeme la Mtera lilifungwa miaka minne iliyopita kutokana na kupungua kwa kina cha maji.