Serikali yasaini makubaliano na Kampuni mbili za CHINA kuanza ujenzi wa daraja la KIGONGO BUSISI.

0
266

Hafla ya utiaji saini ujenzi wa daraja la KIGONGO- BUSISI kati ya serikali ya TANZANIA na Kampuni za China Civil Engineering Construction na China Railway 15 GROUP imefanyika jijini DSM.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi ISACK KAMWELWE ametoa rai kwa wote ambao wamekuwa wakihitaji zabuni bila kufuata taratibu za Mamlaka husika.