Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ametia saini marekebisho ya kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za mwaka 2021, na kupunguza viwango vya tozo za miamala hiyo kwa asilimia 30.
Aidha, Serikali imefanya majadiliano na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza katika miamala ya kutuma na kutoa fedha kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa asilimia 10.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango imeeleza kuwa, viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa tangazo la Serikali kesho Septemba Mosi.
Tarehe 19 mwezi Julai mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan aliwaelekeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Nchemba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile kupitia upya tozo za miamala ya simu baada ya kusikia kilio cha wananchi kuhusu tozo hizo
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.