Serikali yahimiza mpango wa kutoa Elimu ya Masoko na Mitaji

0
264

Serikali imetoa rai kwa mamlaka ya masoko, mitaji na dhamana kuendelea kuboresha mpango wake wa kutoa elimu kwa umma kuhusu uwekezaji katika masoko ya mitaji na dhamana kama sehemu ya kutekeleza jukumu la mamlaka ya kuendeleza masoko ya mitaji hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa shindano la masoko ya mitaji na dhamana Naibu Waziri wa Tamisemi Josephat Kandege amesema kuwa sekta hiyo ni muhimu katika upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa makampuni na hivyo kusaidia umilikishaji kwa umma kwa njia za uchumi.