Serikali yafunga mtambo wa utunzaji wa mazingira

0
141

Wavuvi na watumiaji wengine wa baharini wametakiwa kuwa walinzi wa mazingira ili kukabiliana na uchafuzi wa hewa ya ukaa inayoikabili dunia kutokana na kuwepo kwa asidi nyingi baharini.

Hayo yamesemwa na Dkt. Ishmael Kimirei, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) wakati wa uzinduzi wa mitambo itakatayotumika kupata taarifa ya hali ya hewa na katika bahari ya hidi kwenye mwambao wa Tanzania.

“Ripoti zinaonesha Bahari ya Hindi inaongezeka joto kwa kasi zaidi kuliko bahari zote duniani na joto limeongezeka kwa asilimia 0.88, na hii ni ripoti ya mwaka jana. Tukiondoa mifumo ya ikolojia inayosababisha dunia iwe baridi itasababisha kesho kuwa ngumu zaidi,” ameongeza Dkt Kimirei.

Kwa upande wake Afisa Utafiti TAFIRI, Dkt. Baraka Sekadende amesema mbali na mradi huo wa kuangalia asidi baharini, TAFIRI imeanza kupima ongezeko la vurutubishi maji ili kuwa na samaki wenye afya ambapo kutaongeza tija kwenye mazao ya samaki na kunufaisha wavuvi

Aidha, Mwenyekiti wa Wavuvi Pwani ya Kunduchi, Zedi Mwinyi Zedi ameipongeza serikali kwa mradi huo na kuahidi kuwa wataulinda maana una manufaa zaidi kwenye shughuli zao za uvuvi, hasa kupata taarifa za uvuvi wanapokuwa baharini.

Dunia inakabiliwa na uchafuzi wa mazingira kutokana na hewa ya ukaa kunakopelekea mataifa mbalimbali kutafuta njia za kukabiliana na hali hiyo ikiwepo kupanda miti na usafi wa mazingira kwa ujumla.

Ezekiel Simbeye: