Serikali yafanya mazungumzo na ujumbe kutoka WB na DFID

0
274

Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID).

Wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dodoma, wamejadili kuhusu mradi wa Tanzania Urban Resilience (TURP) unaotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), mradi unaolenga kuzisaidia halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi.

Pamoja na mambo mengine, mradi huo wa TURP ukitekelezwa unatarajiwa kubadili eneo la Mto Msimbazi ambalo limekua likikumbwa na mafuriko kuwa eneo linalofaa kwa ajili ya michezo na lenyemanufaa ya Kiikolojia kwa jiji la Dar es salaam.