Serikali yaboresha Hospitali ya Mirembe

0
136

Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanya maboresho ya miundombinu yaliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 6 katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili-Mirembe.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ujenzi na kuongea na watumishi wa hospitali hiyo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema ujenzi huo umefikia hatua za mwisho hivyo itasaidia wananchi kupata huduma za afya katika mazingira bora

“Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 6 katika kuboresha miundombinu pamoja na vifaa tiba katika hospitali hii, sasa ni jukumu lenu watumishi kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo matumizi ya lugha nzuri,” amesisitiza Dkt. Mollel

Aidha, ameiagiza Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha ndani ya miezi miwili inapeleka vifaa vya upasuaji wa mifupa katika hospitali hiyo ili wananchi waanze kunufaika na huduma hiyo ambayo awali walikua wakiifuata umbali mrefu.