Serikali yabanwa kuhusu mafao ya wastaafu

0
244

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako kutoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya muda mrefu ya mafao ya wastaafu hapa nchini.

Hatua hiyo ya Spika imekuja baada ya Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi kutoa maelezo kuhusiana na hatua ambazo serikali inachukua kutatua mgogoro wa madai ya wastaafu na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Baada ya majibu hayo na yale yaliyotolewa na waziri Ndalichako ndipo Spika wa Bunge akamtaka waziri huyo kutoa maelezo kuhusiana na utatuzi wa mafao ya wastaafu ambayo yamekuwa kero kwa watumishi hao.

“Kutokana na majibu hayo, Mheshimiwa Waziri, nadhani bunge la mwezi Januari mje na maelezo kuhusiana na utatuzi wa suala hili la mafao ya wastaafu ambalo limekuwa kero hata kwetu sisi Wabunge.” amesema Spika